Rais Samia: Nilipowateua Nikki na Mwana FA watu hawakunielewa

Tanga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa uteuzi wa wasanii Hamis Mwinjuma (Mwana FA) na Nickson Simon (Nikki wa Pili) katika nafasi za uongozi umekuwa na manufaa makubwa kwa serikali yake, licha ya mashaka ya awali kutoka kwa baadhi ya watu.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Akizungumza leo, Februari 27, 2025, katika ziara yake mkoani Tanga, ndani ya Jimbo la Muheza ambalo Mwana FA ni mbunge, Rais Samia amesema “Nilipomteua yeye (Mwana FA) na mkuu wangu wa Wilaya ya Kibaha, Nikki wa Pili, watu hawakuelewa.

Wakasema, ‘Mama anateua wachepe hawa, inakwenda kuwaje, hawa wamezoea majukwaa na kurap, watafanya kazi gani? Lakini nataka niwaambie kwamba hawa wananisaidia sana,”.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Aidha, amesisitiza kuwa uwepo wa MwanaFA katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umesaidia sana kufikisha ujumbe kwa vijana kwa lugha wanayoielewa, hivyo kuwaomba wananchi waendelee kumtunza kwa manufaa ya sasa na siku za usoni.

Mbali na wawili hao kuzitumikia vizuri nafasi zao waliwahi kutamba na ngoma kama Safari, Hesabu, Nje ya Box, Gwiji, Mfalme, Bila kukunja goti na nyinginezo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Ikumbukwe Februari 2, 2002, ndio siku ya kwanza kwa wimbo wa kwanza wa Mwana FA kusikika redioni, wimbo huo ‘Ingekuwa Vipi’ alimshirikisha Jay Moe na ulirekodiwa
Mawingu Studio na Bonny Luv ambaye alimsubiri kwa miezi 18 arudi kutoka Uingereza.

Aidha Nikki wa Pili ni mmoja wa wasanii waliounda kundi la Weusi. Kundi ambalo linajifananisha na Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Ureno ambaye bado anacheza soka la kulipwa huko Saudi Pro League katika klabu ya Al Nassr FC licha ya kufikisha umri wa miaka 40.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Sasa idadi ya wasanii wa kundi la Weusi ni sawa na tuzo za Ballon d’Or alizoshinda Ronaldo, pia ni sawa na mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) aliyobeba, ndipo Weusi wakatoa wimbo wao, Ronaldo (2022).