Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ugawaji wa tuzo za wachekeshaji ‘Tanzania Comedy Award’, Jumamosi, Februari 22, 2025 katika ukumbi wa ‘Ware House Masaki’.

Taarifa hiyo imewekwa wazi usiku wa kuamkia leo Februari 27,2025 na Naibu Waziri wa habari tamaduni sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwanafa’, kwenye tamasha la ‘All Stars Comedy Festival’ lililofanyika Mlimani City ikiwa ni utangulizi wa kuelekea siku ya ugawaji wa tuzo hizo.
“Najua hatutegemei kila mtu atakuja, taratibu zinakuwa ngumu kidogo lakini namaanisha kitu kimoja tu kwamba Mtanzania namba moja kwa wakati huu anatambua kazi kubwa inayofanywa na wachekeshaji wetu na ameamua kuunga mkono kwa vitendo kwa kuhudhuria kwenye usiku huo kama mgeni rasmi,” amesema Mwanafa.
Taarifa hiyo imepokelewa kwa furaha na wadau wa sanaa ya ucheshi lakini pia muanzilishi wa tuzo hizo Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ameelezea furaha yake Rais Samia kuwa mgeni rasmi siku hiyo ya ugawaji wa tuzo.
“Kwanza nafuraha sana kwa sababu Serikali imeona kitu hiki ni kikubwa na kuamua kusapoti tasnia hii ya uchekeshaji na kuweza kulipa nguvu wazo Tulilolianzisha.
“Tulipotuma maombi kwa Raisi wetu kama anaweza kuwa mgeni rasmi yeye mwenyewe ni shabiki wa komedi ka bij kiukweli mimi mwenyewe nimefurahi sana kama mnavyoona tumetuma maombi leo na leo leo Rais amekubali kuwa mgeni rasmi,” Amesema Dimpoz.