Rais Samia amelisihi Jeshi la Polisi kujipanga katika kusimamia na kuilinda amani ya nchi kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Amesisitiza kuwa usalama wa wananchi na utulivu wa taifa ni jambo la msingi katika kipindi hicho muhimu cha kisiasa.
Aidha, amelitaka jeshi hilo kudhibiti viashiria vyote vya uvunjifu wa amani mapema iwezekanavyo ili kuzuia madhara makubwa.
#AzamTVUpdates
✍Juliana John
Mhariri | John Mbalamwezi