Rais Biden atoa kauli kugundulika na saratani ya tezi dume

Rais Biden atoa kauli kugundulika na saratani ya tezi dume

Washington. Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden (82), amezungumzia hali yake kwa mara ya kwanza siku mbili tangu agundulike kuwa na ugonjwa wa saratani ya tezi ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake.

Saratani ni ugonjwa unaotokea pindi ukuaji wa seli mwilini unatokea katika namna isiyoweza kudhibitiwa na kuenea kwa kasi, kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Magonjwa la Cancer Research UK.

Rais Biden ambaye anasifika kwa jitihada zake za kupambania uboreshwaji wa miundombinu ya afya duniani wakati wa utawala wake, alibainika kuugua ugonjwa huo Ijumaa ya wiki iliyopita.

Katika chapisho aliloweka jana Jumatatu Mei 19,2025 kwenye akaunti yake ya mtandao wa X huku akiambatanisha na picha yake na mkewe, Jill, Rais huyo ameandika;

“Saratani inatugusa wote kama ambavyo watu wengi wamegundulika kuugua ugonjwa huu. Suala hili limenifundisha mimi na Jill (mkewe) kuwa imara zaidi kwenye nyakati ngumu. Tunawashukuru kwa upendo wenu na kuwa pamoja nasi.”

Awali, taarifa kutoka ofisi ya Biden, ilisema kiongozi huyo aliyeondoka madarakani Januari 2025, alibaini Ijumaa kuwa na ugonjwa hui, baada ya kuonana na daktari wiki iliyopita kutokana na dalili zilizojionesha katika njia ya mkojo.

Ofisi yake iliongeza kuwa saratani aliyokuwa nayo Biden haiathiriwi na homoni, hivyo inaweza kudhibitiwa.

Katika taarifa ya Jumapili ya Mei 18, ofisi ya Biden ilieleza: “Siku ya Ijumaa, aligunduliwa na saratani ya kibofu, yenye alama ya Gleason ya 9 (Daraja la 5) na metastasis kwenye mfupa.”

Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa mashirika ya habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *