Raia waliotoroka Khartoum waanza kurejea baada ya jeshi kuchukua udhibiti

Mamia ya wakimbizi kutoka Sudan, waliokimbilia jijini Cairo nchini Misri, wanatumia usafiri wa mabasi kurejea jijini Khartoum, baada ya jeshi kufanikiwa kuwaondoa wanamgambo wa RSF katika jiji hilo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wakimbizi hao waliokimbia makaazi yao tangu Aprili mwaka 2023, wanasema wana imani usalama umeanza kurejea jijini Khartoum na ni wakati wa kurejea nyumbani.

Siku ya Jumanne, mabasi zaidi ya 200 yaliyokuwa yamewabeba wakimbizi hao, yalionekana jijini Khartoum,  huku mengine yakiwarejesha raia wa nchi hiyo katika majimbo ya Al-Jazeera na  Sinnar.

Hatua hii inakuja baada ya jeshi kuwahimiza watu waliokuwa wameyakimbia makaazi yao jijini Khartoum kuanza kurejea nyumbani, na kuahidi kuwapa msaada wa usafiri.

Wakati hayo yakijiri, aliyekuwa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kusaidia pande zinazopigana nchini Sudan, kutekeleza mpango wa mazungumzo yaliyowahi kufanyika jijini London, ili kumaliza mzozo unaoendelea.

Hamdok, amesema amani ya kudumu nchini Sudan haiwezi kupatikana kwa matumizi ya kijeshi, wito alioutoa kuelekea mkutano wa kimataifa kuhusu namna ya kuisaidia nchi hiyo kupata misaada ya kibidamu, uliopangwa kufanyika jijini London tarehe 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *