
Umoja wa mataifa umesema takribani wanaume, wanawake na watoto Elfu themanini kutoka DRC wamekimbilia nchi jirani kufuatia vita vya Uvamizi, ambapo watu wasiopungua elfu sitini na mmoja wamewasili Burundi tangu Januari mwaka jana.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Msemaji wa umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, amesema watu karibu elfu 17 wamesalia katika makambi ya muda, shume na makanisa huku zaidi ya laki 4 wamekuwa wakihamahama katika kipindi cha wiki nne, wakilazimishwa kufanya hivyo na waasi wa M23.
Dujaric ameongeza kuwa watu kama laki mbili waliotoroka maeneo ya Masisi, Nyiragongo na Rutshuru, ambao walirejea manyumbani kwao baada ya kuwa wakimbizi wa muda mrefu hawana misaada yoyote wa huduma za kimsingi, hali ambayo imewafanya baadhi kuvuka mipaka ili kupata ulinzi na usaidizi.
Soma piaRaia zaidi ya Elfu 60 wa DRC wakimbilia usalama nchini Burundi
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) limetoa wito kwa mataifa yanayoendelea kuwapokea wakimbizi kutoka DRC, kuwasajili waomba hifadhi wote na kuwapa hati ya ukimbizi.