
Raia walionaswa katika mapigano kwenye mji wa El-Fasher nchini Sudan, wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu, wameonya watetezi wa haki za binadamu ambao wamesema hali kwenye mji huo inazidi kuwa mbaya kufuatia miezi kadhaa ya mashambulio ya wapiganaji wa RSF.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na ripoti ya kundi la kutetea haki za binadamu the Darfur General Coordination of Camps for the Displaced and Refugees, raia wa eneo hilo la Elfasher wanakikabiliwa na njaa,magonjwa na ukame wakati huu milio ya makombora na mizinga ikisikika eneo hilo.
Tangu Aprili mwaka wa 2023 Vikosi vya RFS vimechukua sehemu kubwa ya eneo la Darfur isipokuwa eneo la El-Fasher liliko Darfur Kaskazini huku bei za bidhaa zikiogezeka na ukosefu wa pesa ukishuhudiwa .
Makundi yanayounga mkono RSF Sudan Liberation Army na the Gathering of Sudan Liberation Forces mwishoni mwa juma yalitoa wito kwa raia wa El-Fasher na kambi zilizo karibu za Abu Shouk na Zamzan kuondoka, na kuonya kuongezeka kwa operesheni za kijeshi