“Qatargate”: Qatar ‘si nchi adui,’ anasema Benjamin Netanyahu

Qatar “si adui” wa Israeli, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitangaza Jumatano, Aprili 2, akiwatetea washauri wake wawili wa karibu kizuizini kwa tuhuma za rushwa katika kile kinachojulikana kama “Qatargate”.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Qatar ni nchi tata, si nchi rahisi, lakini si nchi adui, na wengi wanaisifu” katika Israeli, kama viongozi kadhaa wa upinzani au hata “mkuu wa Shin Bet, Ronen Bar mwenyewe,” Bw. Netanyahu alisema katika video iliyotolewa na chama chake cha Likud, akimzungumzia mkuu wa idara ya usalama wa ndani, ambaye hivi karibuni kufutwa kwake na serikali kulizuiliwa na Mahakama Kuu.

“Qatargate”, kashfa nyingine inayotishia Netanyahu na washirika wake wa karibu 

Nchini Israeli, Benjamin Netanyahu alihojiwa kama shahidi na polisi Jumatatu mchana. Muda mfupi kabla, washauri wake wawili wa karibu walikamatwa. Walikaa usiku wao wa kwanza chini ya ulinzi wa polisi katika kile kinachoitwa “Qatargate”, kesi ya utakatishaji fedha na kula njama na nchi inayoshukiwa kuwa nchi ya kigeni.

Ufichuzi kutoka kwa vyombo vya habari vya Israeli unaendelea kujitokeza katika jambo hili linaloitwa “Qatargate”, ambalo linatishia Benjamin Netanyahu na washirika wake wa karibu. Washauri wake wawili waliwekwa kizuizini siku ya Jumatatu. Wanahojiwa kuhusu uhusiano wao na Qatar.

Kulingana na vyombo kadhaa vya habari vya Israeli, watu hao wawili walilipwa kwa nyakati tofauti na Doha ili kukuza sura ya Imarati. Kwa wakati huo huo tu, pia walilipwa na serikali ya Israeli. Mtu wa tatu pia anatafutwa na mahakaam. Lakini mtu huyo anaishi nchini Serbia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *