Qatar yakutana tena na wajumbe wa Kongo na Rwanda, pia yakutana na waasi, duru zinasema

Maafisa wa Kongo na Rwanda wamefanya mazungumzo siku ya Ijumaa, wakati wawakilishi wa M23 wamekutana kando na wapatanishi wa Qatar,  vyanzo viwili kutoka kwa serikali ya Kongo na viwili kutoka kwa waasi vimesema.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Qatar imeandaa duru ya pili ya mazungumzo siku ya Ijumaa kati ya Kongo na Rwanda na kukutana kando na wawakilishi wa M23, waasi wanaoendesha uasi mashariki mwa Kongo, duru nne zimeliambia shirka la habari la REUTERS.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walikutana wiki iliyopita mjini Doha kwa mazungumzo yao ya kwanza tangu waasi wa M23 wafanye mashambulizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuiteka miji ya Goma, Kivu Kaskazini na Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini mwezi Januari.

Mazungumzo kati ya Tshisekedi na Kagame, na mwito wao uliofuata wa kusitisha mapigano, yalitoa mwanga wa matumaini ya kupungua kwa mzozo mkubwa zaidi mashariki mwa Kongo katika miongo kadhaa.

Lakini M23 ilitupilia mbali wito huo, ikisema amani inaweza kupatikana tu kwa mazungumzo ya moja kwa moja na Kinshasa, na kuendelea na mashambulizi yake kwa kuuteka mji wa kimkakati wa Walikale.

Wawakilishi wa M23 wamekutana na wapatanishi wa Qatar huko Doha siku ya Ijumaa na hawakufanya mazungumzo na maafisa wa Kongo au Rwanda pia katika mji huo, vimesema vyanzo, viwili kutoka serikali ya Kongo na viwili kutoka kwa waasi.

Maudhui ya majadiliano hayakuwa wazi. Wizara ya mambo ya nje ya Qatar haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

Kongo, Umoja wa Mataifa na serikali za Magharibi zinasema Rwanda inawasaidia waasi kwa kutuma wanajeshi na silaha.

Kigali imekanusha kusaidia M23, ikisema kuwa vikosi vyake vinajilinda dhidi ya jeshi la Kongo na wanamgambo wa Kihutu wa wanaohusishwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyoua takriban watu milioni 1, wengi wao wakiwa ni kutoka kabila la Watutsi.

Mzozo huo umeibua hofu ya kutokea kwa vita vikubwa zaidi vya kikanda, huku majeshi ya Kongo, Rwanda na Burundi yakiwa yameshiriki katika mapigano hayo.

Kaskazini zaidi, Uganda pia ina maelfu ya wanajeshi mashariki mwa Kongo. Wanasaidia Kinshasa kupambana na wanamgambo wengine lakini wanatazamwa kwa mashaka na Wakongo wengi kutokana na uingiliaji kati wa Uganda katika vita vya zamani dhidi ya serikali ya Kongo na shutuma za wataalamu wa Umoja wa Mataifa mwaka jana kwamba Kampala ilikuwa inatoa msaada kwa M23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *