
Wajumbe wa Kongo na AFC/M23 wako Doha kwa karibu wiki mbili sasa. Wapatanishi wamemba kila upande kufanya ishara ya nia njema ili kuunda maingira mazuri yanayofaa kwa mazungumzo. Kujiondoa kwa kundi la M23 katika mji wa Walikale-centre kunawasilishwa na Qatar na Marekani kama ishara ya kwanza ya uwazi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na taarifa zilizokusanywa na RFI, Kinshasa pia imeitikia wito huu kwa kuachilia angalau watu watano. Utambulisho wao haujawekwa wazi. Shida: vuguvugu la waasi wa AFC/M23 halitambui watu hawa kama wako kwenye orodha ambayo waliwasilisha kwa wapatanishi.
Mbali na tofauti hii, kuna pointi nyingine zinazua utata. Matumizi ya maafisa wa Kongo ya neno “kundi la kigaidi” kurejelea AFC/M23 yanaendelea kuzuia mijadala, kulingana na vyanzo kadhaa vya kidiplomasia. Kipengele kingine cha mvutano kinahusu kesi za kisheria zilizoanzishwa dhidi ya rais wa zamani Joseph Kabila.
Vuguvugu la waasi la AFC/M23 linaamini kuwa kesi hii ni kinyume na hatua za kujenga imani zinazonuiwa kuwezesha mazungumzo. Kwa upande wake, wasaidizi wa Joseph Kabila hawajajibu shutuma hizo lakini wanabainisha kuwa rais huyo wa zamani anafanya kazi kama mtu wa amani na kwamba ataendelea na mashauriano yake katika eneo hilo, hususan na wakuu wa nchi, ili kuchangia katika suluhu la mgogoro huo.