Qatar: Inabidi UN itoe azimio la kuilazimisha Israel iheshimu usimamishaji vita Ghaza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kutoa msaada unaohitajika wa kuzisaidia familia zilizoathirika katika mashambulizi ya kikatili ya Israel huko Ghaza na kuhakikisha kunatolewa azimio ambalo litaulazimisha utawala wa Kizayuni kuheshimu usimamishaji vita.