
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amempongeza Sheikh Naim Qassim kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon na kusema: Kikosi cha Quds kitakuwa pamoja na Hizbullah hadi utakapotokomezwa mti habithi wa Uzayuni na kukombolewa Palestina na Quds Tukufu.
Katika ujumbe wake kwa Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu mpya wa Hizbullah ya Lebanon, Brigedia Jenerali Ismail Qaani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa cha Mapinduzi ya Kiislamu, ametoa heshima na kumuenzi Mujahid mkubwa, Shahid Sayyid Hassan Nasrullah, Sahidi Sayyid Hashem Safiyuddin na makamanda na maafisa waliouawa shahidi wa Hizbullah ambao wamepata daraja ya juu la kufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu wakipambana na genge la wahalifu Wazayuni wa Israel.
Amesema katika ujumbe huo kwamba: “Tunatarajia njia ya mwanga na Jihadi ya mashahidi hao itaendelea kwa kasi na nguvu zaidi chini ya usimamizi na uongozi wako.”
Brigedia Jenerali Qaani ameongeza kuwa: Ninakuhakikishia kwamba ndugu zako katika Kikosi cha Quds wataendelea kuwa kandokando yako na pamoja na wapiganaji shupavu wa Hizbullah hadi mti habithi za Uzayuni utakapong’olewa kabisa na Palestina na Quds tukufu itakapokombolewa.
Baraza la Hizbullah ya Lebanon, Jumanne (tarehe 29 Oktoba), lilimtangaza Sheikh Naim Qassem kama Katibu Mkuu mpya wa harakati hiyo.