Putin: Russia itendelea kutoa misaada kwa nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali

Rais wa Russia, Vladmir Putin, amesema nchi yake itaendelea kutoa msaada kwa nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Katika hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Russia na Afrika iliyosomwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov, leo Jumapili katika mji wa Sochi nchini Russia, amesema “Nchi yetu itaendelea kutoa msaada kamili kwa marafiki zetu wa Afrika katika sekta mbalimbali‘.

Putin amesema, Russia inaweza kusaidia nchi za Afrika “maendeleo endelevu, mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali, kupambana na magonjwa ya mlipuko, matatizo ya chakula na matokeo ya majanga ya kimaumbile.”

Mkutano huo wa siku mbili wa ngazi za juu unakuja baada ya mikutano miwili ya kilele kati ya Russia na Afrika mwaka 2019 na 2023

Kwa upande wake, Lavrov amesema uhusiano wa Russia na Afrika umekuwa ukiimarika zaidi na zaidi.Rus sia inataka kuonyesha kwamba vikwazo vya Magharibi vilivyolenga kuitenga kutokana na mashambulizi yake ya Ukraine, vimeshindwa.

Russia ilikuwa mhusika mkuu barani Afrika enzi za Umoja wa Kisovieti na imekuwa na ushawishi katika bara hilo katika miaka ya hivi karibuni.