Putin akubaliana na mpango wa kusitishwa vita kwa siku 30 ila kwa masharti

Rais wa Urusi Vladimir Putin, amesema anakubaliana na wazo la kusitisha vita nchini Ukraine kwa siku 30, lakini kwa masharti.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Putin amesema wazo hilo ni zuri, lakini kuna maswali yanayopaswa kujadili kuhusu utekelezwaji wake.

Kiongozi huyo wa Urusi, amesema nchi yake itajadiliana na Marekani akiwemo rais Donald Trump waliokuja na pendekezo hilo, kabla ya kutoa maamuzi ya mwisho.

Aidha, Putin amesema mkataba wowote wa usitishwaji vita ni lazima uleta amani ya kudumu na kutatua changamoto za msingi za mzozo huo, huku mojawapo ya sharti ni jimbo linalowania la Kursk kuwa upande wa Urusi.

Putin ametaka wanajeshi wa Ukraine kuondoka katika jimbo hilo au wauawe.

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika uwanja wa mapambano katika vita dhidi ya Urusi
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika uwanja wa mapambano katika vita dhidi ya Urusi AP – Alex Babenko

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambaye nchi yake imekubali pendekezo hilo la Marekani la usitishwaji wa vita, ili kuanza mchakato wa mazungumzo, amesema kwa majibu ya Putin, inaonesha kuwa Urusi haitaki amani na kutaka nchi hiyo kuwekewa vikwazo zaidi.

Marekani ambayo inaongoza mchakato wa kujaribu kupata amani ya kudumu kuhusu mzozo kati ya Ukraine na Urusi, wiki hii ilisema hatima ya pendekezo la usitishwaji wa vita kwa siku 30 upo mikononi mwa Moscow.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *