Poland yafanya uchaguzi wa rais, chini ya mtazamo wa Ulaya

Raia wa Poland wanapiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais siku ya Jumapili, kura ambayo inaonekana kuwa na maamuzi kwa mustakabali wa serikali ya sasa inayounga mkono moja wa Ulaya, pamoja na sheria ya uavyaji mimba na haki za walio wachache, wapenzi wa jinsi moja.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Meya wa Warsaw Rafal Trzaskowski, mwanasiasa wa muda mrefu anayeunga mkono EU, anatarajiwa kupata 30% ya kura, mbele ya mwanahistoria mzalendo Karol Nawrocki aanayetarajiwa kupata 25% ya kura, kulingana na uchunguzi wa kura za maoni.

Ikiwa makadirio haya yatatokea, wagombea hao wawili watachuana katika duru ya pili iliyopangwa kufanyika Juni 1, katika wakati mgumu kwa Ulaya na kuendelea kwa vita nchini Ukraine, kuongezeka kwa vyama vya mrengo mkali wa kulia na uhusiano mbaya na Washington.

Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa 3:00 usiku kwa saa za Ufaransa na matokeo ya muda ya uchaguzi yatatangazwa muda mfupi baadaye.

Jumla ya wagombea urais 13 wako kwenye kinyang’anyiro na matokeo ya mwisho yanatarajiwa siku ya Jumatatu.

Tangu muungano wa kiongozi wa zamani wa Umoja wa Ulaya Donald Tusk uingie madarakani mwaka 2023, mipango muhimu ya serikali mara nyingi imepingwa na Rais wa kihafidhina anayemaliza muda wake Andrzej Duda.

Siasa za kimataifa kwa kiasi kikubwa zilitawala kampeni ya uchaguzi, hasa suala la nafasi ya Warsaw kati ya EU na Marekani, na kuangazia mgongano kati ya dhana mbili tofauti.

“Hizi ni chaguzi muhimu sana, ambazo zinapingana na maono mawili yanayokinzana pingana kabisa ya Poland (…): kwa upande mmoja, Poland ya kidemokrasia, Ulaya, wazi, salama na mwaminifu, na kwa upande mwingine, kinyume kabisa,” Marcin Woloszynski, mwanauchumi mwenye umri wa miaka 42, ameliambia shirika la habari la AFP baada ya kupiga kura huko Warsaw.

Masuala ya kijamii pia yalichukua nafasi muhimu katika mijadala ya uchaguzi.

Chama cha Sheria na Haki (PiS), ambacho kinamuunga mkono mzalendo Karol Nawrocki, mara nyingi kilibaki katika mzozo na washirika wa Magharibi wa Poland na Brussels kuhusu masuala ya utawala wa sheria hadi kilipopoteza mamlaka mnamo 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *