Poland: Mgombea wa Kihafidhina Karol Nawrocki ashinda uchaguzi wa urais

Mgombea wa kihafidhina Karol Nawrocki ameshinda uchaguzi wa urais nchini Poland kwa 50.89% ya kura dhidi ya meya wa kiliberali wa Warsaw, Rafal Trzaskowski, kulingana na matokeo rasmi yaliyotolewa leo Jumatatu, na kutoa pigo kubwa kwa serikali ya nchi hiyo inayounga mkono Ulaya.

Imechapishwa:

Dakika 4 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, Karol Nawrocki, akiungwa mkono na chama cha Nationalist Law and Justice (PiS), amepata 50.89% ya kura, ikilinganishwa na 49.11% ya Rafal Trzaskowski, meya wa mji mkuu Warsaw na mshirika wa Waziri Mkuu Donald Tusk. Rais wa sasa wa kihafidhina Andrzej Duda amempongeza mara moja mshindi. “Hongera kwa mshindi!” ameandika kwenye ukurasawake wa Twitter, akiwashukuru Wapoland kwa kushiriki uchaguzi kwa kiwango cha 71.63%.

Karol Nawrocki, 42, bondia mahiri aliyevutiwa na mawazo ya vuguvugu la Rais wa Marekani Donald Trump la “Make America Great Again” (MAGA), aliendesha kampeni kwa ahadi ya kuhakikisha kwamba sera za kiuchumi na kijamii za nchi hiyo zinawapa nafasi kubwa raia wa Poland kuliko raia wa mataifa mengine au wakimbizi, kama vile wale waliokimbia nchi jirani ya Ukraine. Alizaliwa katika mji wa bandari wa Gdansk, ambapo alicheza soka na ndondi katika ujana wake, kabla ya kupata shahada ya PhD katika historia na MBA. Alikuwa mkurugenzi wa Makumbusho ya Vita vya Pili vya Dunia vya jiji kutoka mwaka 2017 hadi mwaka 2021. Tangu mwaka 2021, ameongoza Taasisi ya Kumbukumbu ya Kitaifa (IPN), ambayo inachunguza uhalifu wa Kinazi na Kikomunisti.

Mshabiki wa Trump

Karol Nawrocki ambaye ni mshambiki wa Donald Trump, alikutana naye Ikulu muda mfupi kabla ya duru ya kwanza. Anadai rais wa Marekani alimwambia, “Utashinda.” Mkutano huu ulizua shutuma nchini Poland kwa kuingilia kwa Marekani katika uchaguzi. Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani Kristi Noem alimuunga mkono Nawrocki katika mkutano wa kihafidhina nchini Poland mwishoni mwa mwezi Mei. “Lazima awe rais mtarajiwa,” alisema.

Kwa kauli mbiu yake “Poland kwanza, Wapoland kwanza,” alilenga Umoja wa Ulaya na wakimbizi milioni kadhaa wa Ukraine wanaoishi nchini Ukraine, mwanachama wa EU na NATO. Kama aliahidi kudumisha uungaji mkono wa Poland kwa nchi jirani ya Ukraine, ambayo inapigana na jeshi la Urusi, Karol Nawrocki anapinga uanachama wa nchi hiyo katika NATO na anashutumu misaada inayotolewa kwa wakimbizi wa Ukraine nchini Poland.

Wakimbizi wa Ukraine walengwa

Katika video, ametangaza kwamba manufaa ya kijamii “yalikusudiwa kimsingi kwa raia wa Poland” na kwamba, “katika foleni kwa kutaka kuwaona madaktari na hospitalini,” raia wa Poland ndio wanapaswa “kuwa na kipaumbele.” Pia ameikosoa Kyiv kwa “kutoonyesha shukrani kwa kile ambacho Wapoland wamefanya,” na akamshutumu Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa “ufidhuli” dhidi ya Poland.

Wakati wa kampeni, Karol Nawrocki alitetea kutekelezwa kwa udhibiti wa mpaka na Ujerumani ili kuzuia kuingia kwa wahamiaji, ambao alisema walikuwa wakirudishwa na nchi hiyo, na kuitaka Berlin kulipa fidia ya Poland kwa Vita vya Pili vya Dunia. Kwa matumaini ya kuwatia moyo wapiga kura wa siasa kali za mrengo wa kulia, Nawrocki alitia saini ahadi zilizotayarishwa na kiongozi wao, Slawomir Mentzen.

Kampeni yake ilitawaliwa na ufunuo kuhusu maisha yake ya zamani. Ripoti za vyombo vya habari zilifichua kwamba alinunua nyumba kutoka kwa mzee mmoja katika shughuli iliyochukuliwa kuwa isiyoeleweka na waangalizi na wapinzani wake wa kisiasa. Tovuti ya habari, Onet.pl, pia ilichapisha uchunguzi mkali unaodai kwamba alihusika katika kuleta makahaba katika hoteli moja huko Sopot (kaskazini) alipofanya kazi huko kama mlinzi miaka ishirini iliyopita. Alikanusha madai hayo, akiita uchunguzi huo “lundo la uongo.”

Wakati bunge la Poland linashikilia mamlaka mengi, rais anaweza kupinga miswada ya sheria. Uchaguzi huo ulitazamwa kwa karibu na Ukraine na Urusi, pamoja na Marekani na kote katika Umoja wa Ulaya.

Ongezeko la Matumizi ya Ulinzi

Rafal Trzaskowski na Karol Nawrocki wote wameelezea haja ya kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya ulinzi, wakati Donald Trump anaitaka Ulaya kuwekeza zaidi katika eneo hili na kuendelea kuiunga mkono Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi. Hata hivyo, wanatofautiana katika mtazamo wao wa usalama: wakati Rafal Trzaskowski anazingatia uanachama wa Ukraine katika NATO, ambayo Poland ni mwanachama, muhimu kwa usalama wa taifa, Karol Nawrocki ameelezea upinzani wake, akitaja hatari ya migogoro ya moja kwa moja na Urusi.

Karol Nawrocki ameonyesha uchaguzi huo kama kura ya maoni kuhusu muungano wa serikali ya Donald Tusk anayeunga mkono Ulaya, ambaye Jukwaa lake la Kiraia lilichukua mamlaka miezi kumi na minane iliyopita. Rafal Trzaskowski, 53, aliahidi kumsaidia Donald Tusk kutekeleza mageuzi ya kidemokrasia ambayo amefanya, ambayo wanasiasa wote wawili wanaonyesha kama inahitajika kurekebisha uharibifu uliosababishwa na PiS.

Chama, kilichoshindwa katika uchaguzi wa bunge wa Oktoba 2023 baada ya takriban muongo mmoja madarakani, kilitekeleza mageuzi ya mahakama ambayo yalipingwa hasa na Brussels, ambayo iliyaeleza kuwa kinyume na viwango vya kidemokrasia vya Umoja wa Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *