Zanzibar. Leo Februari 14,2025, ikiwa ni siku rasmi ya kufunguliwa kwa Tamasha la muzuki la Sauti za Busara 2025, Ngome Kongwe, Stone Town kisiwani Unguja. pilikapilika zimeshamiri kisiwani hapa. Ambapo wadau wa muziki kutoka mataifa mbalimbali wamejumuika kuwashuhudia mastaa watakaolipamba jukwaa hilo.

Maandalizi yakiwa yemetaradadi, wasanii wa ngoma nao wakipasha vifaa vyao kwa ajili ya kujiandaa kutoa burudani. Mashabiki pia wanaonekana kufurika viwanjani hapa kadri muda unavyozidi kwenda.
Ikumbukwe kuwa tamasha hilo la msimu wa 22 litafanyika kwa siku tatu mfululizo, kuanzia leo Februari 14 hadi 16,2025. Linatarajiwa kuwapandisha jukwaani wasanii wa ndani na nje ya nchi.
Kati ya wakali wa muziki watakaoshiriki jukwaa ni mwanamuziki wa Hip-Hop nchini Frida Amani ambaye atakuwa msanii wa kwanza wa kike wa Hip-hop kutumbuiza katika jukwaa la Sauti za Busara.

Hata hivyo ataungana mastaa wengine kama Thandiswa (Afrika Kusini), Blinky Bill (Kenya), Christian Bella & Malaika Band (Tanzania). Bokani Dyer (Afrika Kusini), The Zawose Queens (TZ/UK).
Kasiva Mutua (Kenya), Zanzibar Taarab Heritage Ensemble (Zanzibar), Leo Mkanyia & Swahili Blues (Tanzania), Boukouru (Rwanda), Tryphon Evarist (Zanzibar), Charles Obina (Uganda) na Baba Kash (Tanzania).

Mbali na hao wasanii wengine watakaoshiriki ni Assa Matusse (Msumbiji), Mumba Yachi (Congo), Nidhal Yahyaoui (Tunisia), Étinsel Maloya (Reunion), WD Abo (Sudan), B.Junior (Mayotte), uKhoiKhoi (Afrika Kusini), Joyce Babatunde (Kamerun) na wengine wengi