#PICHA:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika moja ya trekta ambalo ni kati ya matrekta zaidi ya 500 na Power Tiller 800, aliyoyazindua leo, katika kilele cha Maonesho ya Nane Nane 2024, Nzuguni jijini Dodoma.
Matrekta hayo ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuwa na matrekta 10,000 ifikapo mwaka 2030, ambapo Wakulima wadogo wadogo watakayakodi kwa gharama nafuu.