#HABARI: Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kagera wameungana kwa pamoja kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi wa Kitaifa na Serikali kwa kuendelea kudumisha amani, utulivu, upendano na Maelewano.
Ibada hiyo iliyowakutanisha viongozi wa Dini ya Kikristo na Kiislamu imefanyika katika Kanisa Anglikana Mt. Yohana Kimbugu – Muleba, mkoani Kagera.
Akiongoza Ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Lweru Kanisa la Anglikana Tanzania, Godfrey Mbelwa amesema viongozi wa Dini na Waumini wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa Kitaifa kwani wanafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi Maendeleo.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewashukuru viongozi wa Dini kwa kuandaa maombi ya kumuombea Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyoambatana na Harambee ya Ujenzi ya wa Kanisa Parishi ya Kimbugu, Muleba mkoani Kagera.