Pezeshkian: ECO ni jukwaa muhimu la ushirikiano baina ya nchi za Kiislamu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo wajibu wa kustawishwa uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na amesema: “Jumuiya ya ECO inaweza kuwa jukwaa linalofaa mno kwa ajili ya kuleta maelewano na ushirikiano kati ya mataifa ya Kiislamu.”