PeacePro Afrika yalitaka kundi la BRICS kukomesha maovu ya Israel

Taasisi moja isiyo ya kiserikali barani Afrika ambayo inapigania masuala ya amani, imelitaka kundi la BRICS kuchukua hatua za kuukomeshha ushari na vitendo vya kiovu vya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Taasisi ya PeacePro imesema kuwa, Kundi la BRICS ikiwa jumuiya kubwa inapaswa kuchukua maamuzi na misimamo thabiti na ya wazi kuhusiana na kile kinachojiri katika Ukanda wa Gaza na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel katika ukanda huo.

Amezitaka nchi wanachama wa BRICS kuchukua hatua haraka na kufafanua msimamo wao kuhusu vita vya Gaza. Kulingana na mtandao wa Pars Today, ikinukuu tovuti ya habari ya African Blueprint, taarifa hiyo imesisitiza kushindwa kwa taasisi za kimataifa kusaidia raia na kutekeleza sheria za kimataifa huko Gaza.

Abdulrazaq Hamzat, mkurugenzi mtendaji wa PeacePro, katika taarifa hii iliyochapishwa nchini Nigeria, ametoa wito kwa BRICS kuiwajibisha Israel kwa vitendo na hatuu zake katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu.

Hamzat ameeleza masikitiko yake kutokana na kupuuzwa maazimio ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kutojali kwa Baraza la Usalama na kudhoofisha hatua za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, akisisitiza kwamba taasisi za kimataifa zimeshindwa kuunga mkono utekelezwaji wa sheria za kimataifa.