
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amempokea Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance siku ya Jumapili, Aprili 20, kando ya sherehe za Pasaka, Vatican ilmetangaza, miezi miwili baada ya mkuu wa Kanisa Katoliki kukosoa vikali sera ya uhamiaji ya utawala wa Donald Trump.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Mkutano huu wa faragha” wa “dakika chache” umefanyika “muda mfupi baada ya 5:30 mchana (5:30 saa za Ufaransa)” katika makazi ya Santa Marta, ambapo Papa anaishi huko Vatican. Mkutano huo “umewezesha (wawili hao) kubadilishana salamu zao katika hafla ya Siku ya Pasaka,” Vaticani imesema katika taarifa kwenye Telegram.
Siku moja kabla, JD Vance alizungumza na Kardinali Parolin, Waziri wa Mambo ya Nje wa Papa Francis ambae ni Namba 2 Vatican.
“Ni furaha kukuona ukiwa na afya bora,” JD Vance amemwambia Papa Francis, kulingana na video iliyorushwa na Vatican. “Asante kwa kuwa nami, nakuombea kila siku.” “Mungu akubariki,” amesema tena kabla ya kumpa mkono.
Papa alimkabidhi makamu wa rais wa Marekani zawadi, zikiwemo rozari, tai yenye nembo ya Vaticani na mayai ya chokoleti kwa watoto wake watatu.
Soma piaPapa Francis akosoa hatua ya Marekani kuwafukuza wahamiaji, White yajibu
Mvutano na White House mnamo Februari
Siku ya Jumamosi, JD Vance, ambaye aliingia dini ya Katoliki akiwa na umri wa miaka 35, alipokelewa mjini Vatican na Kadinali Pietro Parolin wa Italia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Papa Francis ambae ni Namba 2 Vaticani.
Mkutano huo “mzuri” ulishughulikia “hali ya kimataifa, haswa katika nchi zilizo na vita, mivutano ya kisiasa na hali ngumu ya kibinadamu, kwa umakini maalum kwa wahamiaji, wakimbizi na wafungwa,” Vaticani imesema katika taarifa.
Mnamo Februari, Papa Francis alikasirisha Ikulu ya White House kwa kulaani, katika barua kwa maaskofu wa Marekani, kufukuzwa kwa wahamiaji wengi kwa amri ya Donald Trump, akieelezea kama “mgogoro mkubwa.”
“Kinachojengwa juu ya msingi wa nguvu, na sio juu ya ukweli wa utu sawa wa kila mwanadamu, huanza vibaya na mwisho wake ni mbaya,” alionya, wakati JD Vance anakusudia kuifanya nchi yake kuwa ngome ya maadili ya kihafidhina kwa kuzuia sana uhamiaji.