Paris mwenyeji wa mkutano mkuu wa kimataifa wa kuratibu vyema misaada kwa Syria

Zaidi ya miezi miwili baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar Al Assad, Ufaransa ni mwenyeji wa mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu Syria leo Alhamisi hii, Februari 13. Lengo: kuratibu hatua za kikanda na kimataifa kusaidia mchakato wa mpito unaoendelea huko Damascus huku mashirika machache yasiyo ya kiserikali yaliyopo nchini Syria yakikosoa vikwazo vya nchi za Magharibi ambavyo bado vina uzito kwa nchi hiyo, yakizituhumu kuchangia kuchochea mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa mkutano mkuu wa kimataifa kuhusu Syria unaofanyika Alhamisi hii, Februari 13 mjini Paris ni wa tatu kufanyika tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar Al Assad mnamo Desemba 8, ni wa kwanza wa aina yake kufanyika barani Ulaya – miwili ya awali ilifanyika Jordan na Saudi Arabia. Mkutano huo umeandaliwa katika muundo unaoitwa “Aqaba” – uliyopewa jina la mji wa Jordani ambao ulikuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza – Utaleta pamoja nchi za G7, nchi nyingi za Ulaya, nchi za Kiarabu, Uturuki na Umoja wa Mataifa.

Malengo makuu matatu yamewekwa kwa ajili yake: kuanzishwa kwa mamlaka ya uwakilishi na mchakato wa mahakama ya mpito nchini humo, pamoja na uhamasishaji wa washirika wote wa Damascus kuboresha misaada kwa Syria.

Zaidi ya mikutano ya kitamaduni kati ya mawaziri wa mambo ya nje, wawakilishi wa mashirika ya kiraia pia walialikwa mapema, siku ya Jumatano, kuunda mapendekezo yao wenyewe, haswa kuhusu suala la mahakama ya mpito. Alhamisi hii asubuhi, semina ya kikazi na wafadhili wa kimataifa pia iko kwenye ajenda.

Ingawa ajenda ya mkutano huo inatarajiwa kuwa na shughuli nyingi, Paris ina nia ya kusema kwamba hii ni hatua moja tu kuelekea kazi ya muda mrefu. Kwa upande wa Syria, moja ya matakwa makubwa zaidi ya mamlaka ya mpito ni kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya utawala wa Bashar Al Assad, ambavyo bado vinaikosesha mambo mengi nchi hii iliyoharibiwa na miaka 13 ya vita.