Papa Leo XIV alielezea chaguo lake la jina la papa kama kujitolea kwa masuala ya kijamii katika kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya viwanda na akili ya bandia siku ya Jumamosi, Mei 10, wakati wa mkutano na makadinali.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Akiangazia “mtindo wa kujitolea kabisa” wa mtangulizi wake Francis, amesema: “Tukusanye urithi huu wa thamani,” akisema kwamba Papa “ni mtumishi mnyenyekevu wa Mungu na ndugu zake, na si kitu kingine chochote.”
Papa Leo XIV, ambaye jina lake halisi la kuzaliwa ni Robert Francis Prevost, amewaeleza makadinali siku ya Jumamosi, Mei 10, chaguo la jina la utawala wake, na kumfanya mmoja wa watangulizi wake, Leo XIII, papa kuanzia 1878 hadi 1903, na kujitolea kwa masuala ya kijamii.
“Papa Leo XIII, pamoja na waraka wa kihistoria wa Rerum Novarum, alishughulikia swali la kijamii katika muktadha wa mapinduzi makubwa ya kwanza ya viwanda,” anaelezea Leo XIV, ambaye uchaguzi wake ulitangazwa siku ya Alhamisi.

“Leo, Kanisa linampa kila mtu urithi wake wa mafundisho ya kijamii katika kukabiliana na mapinduzi mengine ya viwanda na maendeleo ya akili ya bandia, ambayo yanaleta changamoto mpya kwa ulinzi wa utu wa binadamu, haki, na kazi,” mkuu wa Kanisa Katoliki ameongeza. “Ni kwa sababu ninahisi kuitwa kuendelea na hali hii kwamba nilifikiria kuchukua jina la Leo XIV.”
“Urithi wa thamani” wa Francis
Papa Leo XIII alitetea haki za wafanyakazi kupata mishahara ya haki na mazingira salama ya kazi katika kazi iliyopewa jina la Rerum Novarum kuanzia mwaka 1891, iliyofafanua mawazo ya Kanisa kuhusu matokeo ya Mapinduzi ya viwandani.
Wakati wa mkutano siku ya Alhamisi jioni, Mkurugenzi wa idara ya Habari Vatican Matteo Bruni, pia ameeleza kuwa papa mpya amechagua jina lake kwa kurejelea “wanaume, kwa wanawake, kwa kazi zao, kwa wafanyakazi, kwa enzi ya akili ya bandia.”
Akiangazia “mtindo wa kujitolea kabisa” wa mtangulizi wake Francis, Leo XIV pia ametangaza: “tukusanye urithi huu wa thamani,” akizingatia kwamba Papa “ni mtumishi mnyenyekevu wa Mungu na ndugu zake, na si kitu kingine chochote.”
Robert Francis Prevost alichaguliwa kuwa papa siku ya Alhamisi, Mei 8, na mara moja akatangaza jina lake la utawala, Leo XIV. Chaguo la kusisitiza kujitolea kwake kwa masuala ya kijamii katika kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya viwanda.