Papa Francis atimiza miaka 12 madarakani, hatma yake mashakani akiendelea kuugua

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ameendelea kusalia hospitalini akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya kupumua wakati huu akifikisha miaka 12 ya uongozi wake.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Japokuwa madakatari wake wanasema hayuko kwenye hali ya hatari, Papa amekuwa hospitalini kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa, hali inayoendelea kuzuia wasiwasi miongoni mwa waumini wa Kanisa katoliki duniani.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88, alilazwa katika hospitali ya Gemelli huko Rome tangu tarehe 14 ya mwezi Februari mwaka huu kutokana na matatizo ya mfumo wa upumuaji (Pneumonia).

Huu ndio muda mrefu zaidi ambao kiongozi huyo amekuwa hosipitalini
Huu ndio muda mrefu zaidi ambao kiongozi huyo amekuwa hosipitalini © Matteo Minnella / Reuters

Hali ya raia huyo wa Argentina imeripotiwa kuendelea kuimarika, Jumatano ya wiki hii Vatican ikithibitisha kuwa amekuwa na usiku tulivu hospitalini.

Kwa sasa mjadala umeibuka ni lini Papa ataondoka hospitalini, huu ukiwa ndio muda mrefu zaidi kwa kiongozi huyo kuwa hospitalini tangu alipochukua uongozi wa kanisa lenye idadi ya waumini Bilioni 1.4 duniani.

Wataalam wa afya wanasema itamchukua muda wa wiki kadhaa ili kuwa sawa, kutokana na umri wake mkubwa na kujirudia kwa baadhi ya magonjwa, kutokana na athari zinazoweza kutokana na hatuaj ya kutolewa moja ya pafu lake wakati akiwa kijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *