Papa Francis amekuwa na usiku mtulivu kwenye hospitali: Vatican

Vatican imesema kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis mwenye umri wa miaka 88, ambaye anaugua homa ya mapafu, amekuwa na usiku mtulivu hospitalini.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulinagana na Vatican, Papa Francis anaendelea kupumzika hospitalini ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa muda wa siku 13 sasa.

Papa Francis alilazwa kwenye hospitali ya Gemelli mjini Rome tarehe 14 ya mwezi Februari baada ya kukabiliwa na matatizo ya kupumua, hali yake ikiripotiwa kuendelea kudorora na kuzua hali ya wasiwasi kwa waumini wa kanisa Katoliki.

Licha ya tangazo la Vatican kwamba Papa amekuwa na usiku mtulivu, imeelezwa kwamba kiongozi huyo bado yupo kwenye hali hatari.

Madaktari wanasema huenda Papa Francis ataendelea kusalia hospitalini.
Madaktari wanasema huenda Papa Francis ataendelea kusalia hospitalini. REUTERS – Hannah McKay

Kwa mujibu wa Vatican, Papa ameendelea na majukumu ya kanisa akiwa hospitalini. Kanisa Katoliki lina karibia waumini bilioni 1.4 kote duniani.

Waumini wa kanisa Katoliki wamekuwa wakimuombea kiongozi wao mjini Vatican na nje ya hospitali anakopokea matibabu. Madaktari wameonya kwamba huenda Papa akasalia hospitalini na kwamba itamchukua muda kuwa sawa.