Papa Francis afariki dunia, Vatican yatangaza

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

“Leo asubuhi saa 1:35 Askofu wa Roma, Francis, amerejea nyumbani kwa Baba,” Kadinali Kevin Farrell ameandika kwenye ukurasa wa Telegram.

Vatican, makao makuu ya Kanisa hilo duniani, imetangaza kifo hicho, kinachokuja, baada ya Papa Francis, kuonekana kwenye maadhimisho ya Pasaka April 20 2024, kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesema Papa Francis atakumbukwa kama kiongozi ambaye siku zote alikuwa upande wa watu masikini na wanaohitaji msaada.

Historia ya Papa Francis

Papa Francis, amekuwa akiumwa kwa wiki kadhaa na alilazwa hospitalini kwa siku 38 na baadaye kuondoka hospitalini, kabla ya kutokea kwa kifo chake Jumatatu Aprili 21 2025.

Raia huyo wa Argentina, na aliyekuwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires, alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kwa miaka 12 na siku 39.

Alikuwa mzaliwa wa Argentina, na jina lake halisi, ni Jorge Mario Bergoglio.

Mwaka wa 2013, alikuwa Papa wa kwanza wa shirika la Jesuit.

Papa Francis wakati wa uhai wake
Papa Francis wakati wa uhai wake © Gregorio Borgia / AP

Papa Francis anaacha urithi gani?

Wakati wa uhai wake alisafiri kwenda kwenye maeneo ambayo hakuna papa mwingine aliyewahi kufika.

Alikwenda katika kisiwa cha Lesbos au Lampedusa kuonana na wakimbizi, lakini alifika Papua New Guinea.

Pia alitembelea nchi ambazo zinakabiliwa na vita, kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati, au ambazo ziliwahi kushuhudia vita, kama vile Iraq.

Alifika pia kwenye nchi zenye Wakristo wachache, kama vile Burma na Indonesia.

Soma piaVatican: Papa Francis afariki dunia

Kuhusu fedha, aliongoza mageuzi ya kulazimishwa ya Curia, utawala huu mzito wa Kanisa Katoliki.

Hakuwa na marafiki wengi, na mara kwa mara alikosoa utengano kati ya makasisi na waaminifu.

Kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, kulikuwa na mwamko, na kusikiliza zaidi waathiriwa.

Mtindo wake rahisi na wa moja kwa moja utasalia na hamu yake ya kupendelea mazungumzo ili dunia kuwa na amani. Mara kwa mara, alizungumzia ukomeshwaji wa vita kati ya Urusi na Ukraine, ukanda wa Gaza na vita nchini Sudan.

Kwa kipindi cha miaka 12, Papa Francis, ameacha Kanisa thabiti lakini kwa waokoaji wake, wanasema ameacha Kanisa lililogawanyika, kutokana na misimamo yake, ikiwemo kuruhusu wapenzi wa mapenzi ya jinsia moja kubarikiwa.

Papa Francis akifanya maombi wakati wa uhai wake
Papa Francis akifanya maombi wakati wa uhai wake © AP/Andrew Medichini

Nini kinafanyika baada ya Papa kuaga dunia ?

Utaratibu wa kumtafuta kiongozi mpya wa Kanisa hilo, unatarajiwa kuanza kati ya siku 15 hadi 20, ambapo Makadinali watapiga kura.

Makadinali 135 wanatarajiwa kupiga kura, 108 walichaguliwa na Papa Francis. Miongoni mwao ni 18 kutoka barani Afrika.

Kanisa Katoliki, ipo kwenye kipindi kinachoitwa, “Sede Vacante” ambapo Kadinali mwenye cheo cha juu anasimamia shughuli za Kanisa hilo, kabla ya kuchaguliwa kwa Papa mpya.

Makadinali kutoka kote duniani, wanatarajiwa kukutana na kuamua ni lini Papa Francis atazikwa, kwa kawaidi, mazishi hufanyika siku ya nne au ya sita baada ya kifo cha kiongozi mkubwa kama huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *