Papa aanzisha jimbo jipya Bagamoyo, amteua Askofu Musomba kuliongoza

Dar es Salaam. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, Papa Francis amemteua Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Stephano Musomba kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Bagamoyo kuanzia leo Ijumaa, Machi 7, 2025.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima imeeleza Askofu Musomba hadi anateuliwa alikuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam tangu mwaka 2021.

Askofu Musomba amezaliwa Septemba 25, 1969 Malonji jimboni Mbeya. Baada ya masomo yake ya upadri alipewa daraja takatifu la upadri Julai 24, 2003 na kuhudumu katika nafasi mbalimbali za utume shirikani, jimboni Dar es Salaam na Morogoro.

Kwa maana hiyo ongezeko la Jimbo jipya la Bagamoyo kutafanya majimbo ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania kufikia 36.

Endelea kufuatilia Mwananchi.