
PAMBA Jiji itakuwa inakumbuka kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Tabora United mwaka jana katika mechi ya duru la kwanza ya Ligi Kuu Bara, licha ya kwamba tangu kuanza kwa duru la pili timu hiyo imeonekana kuimarika zaidi.
Timu hizo zinatarajiwa kukutana leo ikiwa ni kati ya mechi mbili za Ligi Kuu zinazopigwa leo Jumamosi, huku mshabiki wakitarajia kushuhudia pambano la kiufundi zaidi, Pamba ikitaka kulipa kisasi na kulinda heshima ikiwa nyumbani, lakini Tabora ikitaka kuendeleza ilipoishia baada ya kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Yanga.
Pamba Jiji itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kumbukumbu ya kutoka kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo na inaikabili Tabora iliyotoka kufungwa na Yanga.
Huu utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa Pamba Jiji baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza na makocha wa timu zote mbili wametambiana kila mmoja akisisitiza kuzihitaji pointi tatu.
MASHUJAA vs FOUNTAIN GATE
Ni mchezo wa kusaka heshima kwa timu zote mbili mchezo wa mzunguko wa kwanza ziligawana pointi moja baada ya sare ya mabao 2-2.
Mashujaa itakuwa nyumbani ikisaka pointi tatu muhimu za kurudisha morali kwa wachezaji baada ya kutokuwa na matokeo mazuri kwenye mechi tano zilizopita ikifungwa tatu, sare moja na ushindi mchezo mmoja sawa na Tabora United ambayo pia mechi tano zilizop