
Takriban wanajeshi wanane na raia mmoja waliuawa magharibi mwa Pakistan siku ya Ijumaa katika mashambulizi tofauti kwenye mpaka na Afghanistani, ambapo ghasia zimezuka katika miezi ya hivi karibuni, polisi wameliambia shirika la habari la AFP.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wanajeshi saba waliuawa katika operesheni ya usalama dhidi ya “Taliban waliojihami kwa silaha” kaskazini magharibi mwa mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, chanzo cha polisi kimesema leo Jumamosi.
“Wapiganaji waliokuwa wamejificha kwenye nyumba walivifyatulia risasi ikosi vya usalama,” chanzo hicho kimesema.
Jeshi lilituma helikopta za kivita wakati wa mapigano hayo yaliyodumu kwa saa nyingi, na kuwauwa wapiganaji wanane wa Taliban, huku wanajeshi wengine sita wakijeruhiwa, chanzo kimesema.
Mlipuko wa bomu lililotegwa na watu wanaotaka kujitenga kwenye pikipiki pia uliua mwanajeshi na raia mmoja kusini mwa Balochistan, afisa wa polisi Mohsin Ali ameiambia shirikala habari la AFP.
Eneo hilo lilikuwa eneo la shambulio la kustaajabisha mwezi uliopita wakati wanamgambo waliwashikilia mateka mamia ya abiria wa treni na kuua makumi ya wanajeshi ambao hawakuwa kazini.
Wanajeshi watatu na raia mmoja pia walijeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea wakati gari la kijeshi likipita katika wilaya ya Gwadar, eneo nyeti ambalo huhifadhi miundombinu mikubwa ya China.
Zaidi ya watu 190, wengi wao wakiwa wanajeshi, wameuawa katika mashambulizi tangu mwanzoni mwa mwaka huu na makundi yenye silaha yanayopigana na serikali huko Khyber Pakhtunkhwa na Balochistan, kulingana na hesabu ya shirika la abari la AFP.
Kundi la Taliban la Pakistani — linalojulikana kama Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP) — lilitangaza katikati ya mwezi Machi “kampeni ya masika” dhidi ya vikosi vya usalama.
Mwaka jana ulikuwa mwaka mbaya zaidi kuwahi kutokea katika takriban muongo mmoja nchini Pakistani, huku zaidi ya watu 1,600 wakiuawa katika mashambulizi — karibu nusu yao wakiwa askari wa vikosi vya usalama — kulingana na Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Usalama chenye makao yake mjini Islamabad.
Ghasia hizo kwa kiasi kikubwa zinahusu maeneo ya mpakani mwa Pakistani na Afghanistani.