Pakistani inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na inataka ‘kuiwajibisha India’

India imefanya “mashambulizi 24” kwenye “maeneo sita” nchini Pakistani usiku wa Jumanne, Mei 6, kuamkia Jumatano, Mei 7, ametangaza msemaji wa jeshi la Pakistani, ambaye kwa mujibu wake takriban raia 26 waliuawa katika milipuko hiyo. New Delhi, kwa upande wake, inadai kushambulia “miundombinu ya kigaidi” na imeiita jibu lake “Operation Sindoor” . Pakistani imejibu kwa kurusha makombora katika eneo la India na kusababisha vifo vya takriban watu 12, kulingana na jeshi la India.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

India imefanya mashambulizi ya anga katika maeneo kadhaa ya Pakistani usiku wa Jumanne, Mei 6, kuamkia Jumatano, Mei 7. Miji sita imeshambuliwa, huko Kashmir ya Pakistani na Punjab. New Delhi inasema imelenga “miundombinu ya kigaidi” iliyoko katika ardhi ya Pakistani.

Mashambulizi ya India ni jibu kwa shambulio la kigaidi lililotekelezwa Aprili 22 huko Kashmir inayoshikiliwa na India; Takriban watu 26, wengi wao wakiwa watalii, waliuawa.

Makombora ya India na urushianaji risasi vimesababisha vifo vya raia 26 na kuwajeruhi wengine 46, kulingana na jeshi la Pakistani, ambalo limeongeza kuwa bwawa la kuzalisha umeme huko Kashmir limeharibiwa.

Pakistani inadai “imerusha ndege tano” katika anga ya India, wakati chanzo cha usalama cha India kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba ndege tatu za jeshi la anga zimedondoka kwa sababu zisizojulikana. Kulingana na AFP, kijiji cha Kashmiri cha India cha Poonch ambacho kimekumbwa na mashambulizi kadhaa kimerekodi vifo vya watu 12 na wengine 38 kujeruhiwa, kulingana na chanzo hicho. Milipuko mikali pia imetikisa maeneo jirani ya Srinagar. Ni vurugu kubwa zaidi kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu za nyuklia katika kipindi cha miongo miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *