
KAMA kuna shabiki aliyekuwa akiamini Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli wanatimka Yanga kwa vile mikataba waliyonayo kwa sasa inamalizika mwisho wa msimu huu, basi pole yao.
Pacome na Maxi waliosajiliwa msimu uliopita mikataba yao inaenda ukingoni na kulikuwa na tetesi kwamba mabosi wa Msimbazi walikuwa wakiwapigia hesabu ili kuhakikisha wanavuka mtaa kutua Simba, jambo lililowafanya vigogo wa Jangwani kukimbizana kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa.
Mabosi hao wa Yanga wameamua kumaliza mambo kiutu-uzima kwa kuwaita mezani wachezaji hao na kuwaongezea mkataba wa miaka miwili kila mmoja, ili kuendelea kukipiga katika kikosi hicho.
Maxi aliyesajiliwa kutoka AS Maniema ya DR Congo na Pacome aliyetokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast walisainishwa mikataba wa miaka miwili mara walipotua Jangwani ambayo inamalizika mwisho wa msimu huu.
Mmoja wa viongozi wa Yanga, aliliambia Mwanaspoti kuwa, tayari wachezaji hao wameshasaini mikataba mipya baada ya kufanya nao mazungumzo kwa muda mrefu