Operesheni ya Jeshi la Somalia yaua magaidi 70 wa Al-Shabaab katika jimbo la Hirshabelle

Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza kuwa vikosi vya jeshi vikishirikiana na vikosi vingine vya ndani vimewaua wanamgambo wapatao 70 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika operesheni ya mashambulizi viliyotekeleza jana Jumanne katika maeneo kadhaa ya jimbo la Hirshabelle kusini mwa katikati ya nchi hiyo.