Onyo la Iran kwa Troika ya Ulaya kwa kukiuka Azimio la Umoja wa Mataifa na JCPOA

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yaliyoko mjini Vienna, ametoa indhari kwa Troika ya Ulaya kuhusiana na ukiukaji wake wa Azimio la Umoja wa Mataifa na la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA.