Ofisi ya siasa na walinda amani wa UN katika tuhuma za unyanyasaji wa kingono

Madai ya unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji katika ujumbe wa kulinda amani na ule wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa, vimeshika nafasi ya 100 kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka 10 iliyopita hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa wiki hii, ikionesha madai 65 kati ya hayo yanahusisha wanawake waliojifungua baada ya kuripoti kubakwa na walikuwa wakitafuta msaada wa watoto wao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema katika ripoti hiyo mbele ya Baraza Kuu kwamba madai hayo yalibainisha waathiriwa 125, miongoni mwao, watu tisini na wanane ni watu wazima na watoto ni ishirini na saba.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, visa vya ubakaji vilivyozidi arobaini na nne vilihusisha wafanyakazi wa UN 44 katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliotumwa Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na zaidi ya arobaini katika ujumbe wa UN uliotumwa Jamhuri ya Afrika ya kati.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. © FABRICE COFFRINI / AFP

Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu umekuwa ukiangaziwa juu ya tuhuma za ubakaji wa watoto na unyanyasaji mwingine wa kijinsia unaofanywa na walinda amani wake, haswa wale walio katika nchi hizo mbili za Afrika.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty, limesema hali ukiukwaji wa haki na uhuru wa kiraia imeendelea kushuhudiwa nchini Niger tangu jeshi kuchukua madaraka 2023, ambapo waliahidi kuheshimu haki katika mapambano yao dhidi ya wanajihadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *