Odinga: Sina kinyongo, nimeridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa AUC

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga amesema ameridhishwa na mchakato wa uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), kurithi mikoba ya Moussa Faki Mahamat.