
Hali ya usalama katika mji wa Goma na viunga vyake imezidi kuwa ya wasiwasi tangu waasi wa M23 na Muungano wa Mto Kongo wa Corneille Nangaa, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda kuchukuwa udhibiti wa mji huo. Ripoti ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), iliyochapishwa siku ya Jumanne Februari 25, inabainisha kuongezeka kwa matukio ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara na wizi na watu kushambuliwa na makundi ya watu wenye silaha yakiwakuta numbani.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Matukio haya yanachochea hali ya hofu na wasiwasi miongoni mwa raia, kulingana na OCHA.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa magari ya watu binafsi na mashirika ya kibinadamu, yaliyokamatwa na watu hao wenye silaha, bado hayajarejeshwa.
Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari, ni tishio linaloendelea la vilipuzi ambavyo havijalipuliwa huko Goma na viunga vyake.
Wiki iliyopita, watoto wawili walijeruhiwa na mlipuko wa guruneti katika kitongoji cha Bujovu katika mji wa volcano, na hivyo kuzidisha hali ambayo tayari ilikuwa mbaya.
Kuzorota kwa hali ya afya
Aidha, kwa upande wa afya, OCHA pia inataja kuzorota kwa hali ya afya.
Hospitali kuu sita mjini Goma, zzikisaidiwa na washirika wa kibinadamu, bado zimeelemewa na wimbi la majeruhi.
Kufikia Februari 14, zaidi ya majeruhi 3,000 na vifo 842 vimerekodiwa katika vituo vya afya vya Goma, Karisimbi na Nyiragongo. Vituo hivi vya afya sasa vina hofu ya uhaba wa dawa, ripoti inataja.
Kulingana na tathmini iliyofanywa na shirika la Médecins Sans Frontières siku chache zilizopita, vituo vya afya 34 kati ya 47 katika mkoa wa Kivu Kaskazini viliathiriwa na ghasia.
OCHA pia imeongeza kuwa kesi zinazoshukiwa za ugonjwa wa kipindupindu zimeripotiwa katika kambi ya MONUSCO iliyoko Goma, ambako wanajeshi wengi waliopokonywa silaha kutoka katika Jeshi la DRC (FARDC) wamekimbilia hapo.
Kufikia sasa, kifo kimoja kutokana na kipindupindu kimerekodiwa, na wagonjwa 24 wanaoshukiwa wanatibiwa.
Vipimo vya uchunguzi wa haraka vilithibitisha kesi tatu kati ya magonjwa hao.
Katika kukabiliana na mlipuko huu unaowezekana, Shirika la Afya Duniani (WHO) limeweka hatua za kukabiliana na ugonjwa huo.
Kikundi cha afya kimeonya juu ya kuongezeka kwa mlipuko wa kipindupindu ndani na karibu na Goma, huku wagonjwa 420 na kifo 1 kikiripotiwa kwa wiki mbili mfululizo.