NYEPESI NYEPESI ZA DABI: Dabi za sasa hazina undava

KAMA wewe ni mtoto wa 2000, huenda hii inaweza kuwa ngumu kuamini, lakini ukweli ni Dabi ya Kariakoo kwa sasa haina undava kabisa, kwani mabeki wamekuwa laini tofauti na miaka ya nyuma. Miaka ya 1980 kulikuwa na vita baina ya washambuliaji dhidi ya mabeki wa timu hizo. 

Zamoyoni Mogella na Zubeir Magowa wanaweza kuwa shahidi alivyopata upinzani mbele ya mabeki Athuman Juma ‘Chama’ na Yusuf Ismail ‘Bana’ na wakati mwingine hadi kwa kipa Hamis Kinye.

Miaka ya 1990 kulikuwa na vita nyingine ya Edibily Lunyamila na Abukabar Kombo, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ dhidi ya George Masatu, kiasi kila ilipofika dabi, ilikuwa lazima kiwake. Sijakuambia ile vita ya Dua Said na Bakar Malima ‘Jembe Ulaya’ waliozimishana uwanjani. Dabi za sasa hazina ubabe kabisa!