
Norway itamrejesha nchini Rwanda mtu mmoja kwa ombi la nchi hiyo ya Afrika Mashariki, kujibu mashtaka ya mauaji wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, polisi wa Norway walisema Jumanne.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Mahakama ya wilaya ya Oslo iliamua mnamo mwezi Septemba 2023 kwamba masharti ya kurejeshwa nyumbani yametimizwa, na mahakama kuu ya Norway mnamo mwezi Juni mwaka jana ilithibitisha uamuzi huo baada ya mshtakiwa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa awali, polisi imesema katika taarifa.
Wizara ya sheria ya Norway iliamua Februari 14 kwamba mtu huyo, ambaye alikamatwa katika nchi hiyo ya Nordic mwaka 2022, apelekwe Rwanda, ikitaja wajibu wake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya Umoja wa Mataifa kufanya hivyo, polisi imeongeza.