
Pars Today-Watumiaji wa mtandao wa kijamii X wametuma jumbe mbalimbali kwenye mitandao ya intaneti kulaani jinai zinazofanywa utawala wa Kizayuni nchini Lebanon.
Kufuatia jinai za hivi karibuni za utawala wa Kizayuni nchini Lebanon, tumeamua kutupia jicho hisia zilizoonyeshwa na mijibizo iliyotolewa na watumiaji wa mtandao wa X dhidi ya unyama na uhayawani wa utawala khabithi wa Kizayuni.
Muqawama hautakwisha
“Sayyid Mohammad Hossein Mirlowhi”, mwanaharakati wa mtandao wa kijamii wa X ameandika yafuatayo kwenye mtandao huo katika mjibizo wake kwa mauaji ya viongozi wa Muqawama vya Lebanon yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni:
“Kuna siku Hizbullah ilikuwa na mamia tu ya wapiganaji. Ukiondoa silaha za binafsi, ilikuwa na idadi Fulani tu ya maroketi ya Katyusha na Maguruneti. Mtaji wake wote ulikuwa ni Imad Mughniyah; wakamuua shahidi. Lakini sio tu Hizbullah haikwisha … ilipata maelfu ya maelfu ya wapiganaji, na hivi sasa ina silaha za kimbinu za binafsi na makombora bora kabisa ya kuangamiza yanayoongozwa na mitambo”.
Utawala khabithi unavuta pumzi zake za mwisho
Mtumiaji wa mitandao aitwaye “Maede Zaminii” yeye amegusia namna utawala wa Kizayuni unavyotapatapa katika kukabiliana na kambi ya Muqawama na akaandika:
“Angalia hali ya Hizbullah ya Lebanon, makundi ya Muqawama na utawala wa Kizayuni ilivyokuwa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita ili ujue ni kitu gani kinaufanya utawala wa Kizayuni uhamaki na kukasirika. Utawala huo khabithi unavuta pumzi zake za mwisho, na inshallah mara hii utaangamia moja kwa moja. Na alhamdulillah, uchipukaji wa mbegu mpya katika kambi ya Muqawama ni mkubwa sana kiasi kwamba mauaji hayataufikisha utawala huo popote.”
Utawala muuaji wa watoto sasa umefikia kwenye hali mbaya sana
Fouad Izadi, mtaalamu wa masuala ya kimataifa, yeye pia ameandika yafuatayo kwenye mtandao wa kijamii wa X:
“Baada ya miaka 76 ya operesheni za kigaidi, utawala muuaji wa watoto sasa umefikia kwenye hali mbaya sana. Mauaji hayajawa na wala hayatakuwa wenzo wenye ufanisi kwa utawala huu.”
Tuueni sisi ili umma uzidi kuamka
Ahmad Bastami, mmoja wa watumiaji wa mtandao wa kijamii X, ameandika:
“Katika historia ya mapambano yake dhidi ya utawala ghasibu, Hizbullah imepitia tajiriba ya kuuliwa makamanda wake wengi na hata Katibu Mkuu wake Abbas Mousavi, lakini je, waliweza kuisimamisha Hizbullah? Sio tu hawakuweza, lakini Hizbullah iliendelea kila siku kuwa na nguvu zaidi. Kwa hiyo tunasema maneno yaleyale ya Imamu (Khomeini) kwamba “Tuueni sisi ili umma uzidi kuamka”.
Inapasa Wazayuni watawaliwe na khofu
Reza Abedi Gonabadi, mmoja wa wanaharakati wa mtandao wa kijamii wa X, yeye amesema:
“Njia pekee ya kukomesha jinai za Israel ni kushambulia miji mikubwa na kuwatia hasara ya maafa makubwa. Hakuna njia nyingine, lazima khofu iwatawale Wazayuni. Katika hali hii hata Marekani na Magharibi ambazo ni waitifaki wa utawala huu zitasalimu amri.”
Wazayuni ni wapumbavu
“Mehdi Mohammadi” ameandika hivi kwenye mtandao wa kijamii wa X:
“Kila unachokiona ni “pendekezo la kusalimu amri” Hizbullah. Wazayuni hata wawe wauaji mahiri na stadi kiasi gani, watabaki kuwa ni wapumbavu!”