

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wengi mara nyingi hupata baridi wakati wa msimu wa masika na ugumu wa kupumua kwa sababu ya pua iliyoziba.
Kwa kushindwa kupumua kupitia pua, wengine hupumua kwa kutumia kinywa. Na, je, ni vizuri kupumua kupitia mdomo? Nini kitatokea ukifanya hivi? Wacha tuone wataalam wanasema nini.
Kwa wastani tunapumua lita 10,000 hadi 12,000 za hewa kwa siku. Hewa hii pia ina vumbi, bakteria, virusi na kuvu. Hizi husafiri kwenye njia yetu ya upumuaji na kufikia mapafu.
Hata hivyo, hatuhitaji kuwa na wasiwasi kuhusu hili. Mfumo wetu wa kupumua unajua jinsi ya kusafisha uchafu huu.
Kupitia mfumo wa upumuaji, ni chembe chembe ndogo tu chini ya mikroni tatu ambazo zinaweza kuingia kwenye mapafu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je, mfumo wetu wa upumuaji unachuja vipi uchafu na vijidudu tunavyovuta pamoja na hewa? Ili kujua jibu swali hili, kwanza tunahitaji kujua kuhusu mashujaa wanaoitwa “Cilia”.
Cilia ni miundo myembamba ya nywele. Ni nyembamba kuliko ncha ya sindano.
Kuna maelfu ya nywele hizi kwenye njia zetu za upumuaji. Kati ya 25 hadi 35 ya cilia hizi hupatikana kwenye kila seli ndani ya pua. Zina urefu wa mikroni tano hadi saba kila moja.
Zinapatikana kwenye seli, na huonekana kama brashi. Kazi yao ni kuzuia kupenya kwa viumbe vidogo ambavyo ni chini ya 0.5 mm kwa upana.
Matokeo yake, huchuja viini vidogo vidogo na kuvitoa kupitia pua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vichujio katika pua
Kwa upande mwingine, tishu kwenye pua pia hutumika kuchuja vijidudu vya hewa. Kamasi iliyopo pia inaruhusu baadhi ya viini kuingia mwilini. Kimsingi huruhusu vijidudu visivyo na madhara ndani ya mwili wetu.
Hata hivyo, IAGs, kingamwili zinazozalishwa na seli za aina-B, zina jukumu kubwa katika kuzuia viini hatari vinavyovuka kupitia kamasi na kuingia mwilini.
Je nini hutokea unapopumua kupitia kinywa chako?
Jukumu kuu la kinywa ni ulaji wa chakula. Hakuna cilia zinazoonekana mdomoni ili kuchuja hewa.
Hata hivyo, mfumo huu huzuia vijidudu kutoka kwa chakula kuathiri mwili wetu.
Ndiyo sababu hatupaswi kula chakula kupitia pua zetu. Hivyo basi, usivute hewa kupitia mdomo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nini hufanyika unapopumua kwa mdomo kwa muda mrefu?
Baadhi ya watu hupumua kupitia kinywa kutokana na mabadiliko fulani ya kijeni pamoja na matatizo ya njia ya hewa kwenye pua.
Kupumua kwa kinywa husababisha matatizo ya usingizi.
Hata hivyo, utafiti uligundua kuwa mifupa usoni mwa watoto ambao walipumua kwa muda mrefu kupitia midomo yao iliathirika.
Imedaiwa katika utafiti kwamba husababisha matatizo katika ukuwaji wa mifupa na meno.
Kwa watu wazima, hata hivyo, kupumua kwa kutumia kinywa kunaweza kusababisha maumivu ya misuli ya uso na shingo pamoja na maumivu ya kichwa.
Mwaka 2020 utafiti ulifanywa na Baraza Kuu la Vyuo vya Madaktari wa Meno na Stomatologists nchini Uhispania juu ya upumuaji wa kutumia mdomo.
Utafiti huo ulibaini kuwa nusu ya watoto wenye umri wa miaka 12 waliohusika walikuwa na matatizo ya meno.
Utafiti huo huo pia uligundua kuwa miongoni mwa watu wazima, shingo zinaweza kulazimika kuinama mbele kidogo ili kupumua, na kusababisha mshtuko wa misuli.
Ikiwa una shaka yoyote juu ya faida za kupumua kwa pua, jaribu kupumua kwa mdomo.
Ikiwa kupumua kwa pua ni suala la kawaida, kupumua kwa mdomo husababisha shinikizo au athari fulani mwilini.
Hata hivyo, wataalam wanapendekeza kwamba unaweza kupumua kwa mdomo tu katika hali ya dharura.
Imetafsiriwa na Seif Abdalla na kupitiwa na Asha Juma