Nigeria: Zoezi la kufungwa kwa kambi za wakimbizi wa ndani za Maiduguri linaaendelea

Nchini Nigeria, gavana wa Jimbo la Borno (kaskazini mashariki), kitovu cha uasi wa wanajihadi kwa zaidi ya miaka kumi na tano, ametembelea kambi kubwa zaidi ya watu waliokimbia makazi yao katika jimbo hilo siku ya Jumatatu, Mei 5. Babagana Zulum amebaini kwamba kambi ya Muna itafungwa kabisa katika wiki zijazo. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka wa 2021, gavana wa Jimbo la Borno amejiwekea lengo la kufunga rasmi kambi zote za wakimbizi wa ndani katika mji wa Maiduguri, ambaonazaidi ya 80% ya karibu watu milioni mbili waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo kati ya jeshi la Nigeria na Boko Haram. Lakini mkakati huu ni mgumu kutekelezwa huku hali ya usalama ikizorota tena kaskazini mashariki mwa Nigeria.

“Boko Haram haitatokomezwa kamwe bila kuwarejesha makwao raia waliokimbia. Watu lazima warudi majumbani mwao na kujipatia riziki,” gavana wa Jimbo la Borno aliwaambia watu waliokimbia makazi yao katika kambi ya Muna siku ya Jumatatu, Mei 5. Kati ya mwaka 2021 na 2024, serikali ya jimbo hili la Nigeria ilifunga rasmi kambi kumi na saba karibu na jiji la Maiduguri. Hii imeathiri karibu watu 167,000, kulingana na takwimu zilizomo katika ripoti ya hivi karibuni ya Norwegian Council Institute.

Mchakato unaokwenda kwa mwendo wa kinyonga kutokana na mafuriko

Kambi ya Muna ni kambi kubwa zaidi katika eneo hilo, ikiwa na kaya 10,000 zilizorekodiwa mwanzoni mwamwaka 2024. Siku ya Jumatatu, Gavana Babagana Zulum amebaini kwamba familia 6,000 tayari zimepewa makazi mapya na kwamba kambi hiyo itafungwa kabisa katika wiki zijazo. Mchakato huu unakwenda kwa mwendo wa kijikokota kutokana na mafuriko makubwa ambayo yalikumba Jimbo la Borno mnamo mwezi wa Septemba 2024, lakini gavana amesema uhalifu ndani ya kambi ya Muna unahitaji hatua za haraka.

Watu waliokimbia makazi yao watapata usaidizi wa kati ya euro 25 na 50 na wataweza kurejea vijijini mwao au kuishi katika maeneo yanayochukuliwa kuwa “salama” na mamlaka. Lakini wachunguzi wa kimataifa wanaamini kuwa makazi mapya mengi hayafikii viwango vya chini vya kurudi kwa “hiari, salama, na heshima”, na kwamba njia hii imesababisha kuibuka kwa maeneo ya papo hapo na kuongezeka kwa shinikizo kwa kambi zilizopo, kwani shughuli za wanajihadi zimeongezeka tena tangu mwanzoni mwa mwaka 2025.

Makazi mapya ndani ya miaka mitatu ijayo

Serikali ya jimbo la Borno inakadiria kuwa dola bilioni 2.7 zitahitajika ili kuhakikisha makazi mapya ya watu wote waliohamishwa kutoka kambi rasmi za Maiduguri ndani ya miaka mitatu ijayo chini ya “Mkakati huu wa Jimbo la Borno.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *