Nigeria: Zaidi ya watu Elfu 6 watoroka makazi yao baada ya shambulio

Nchini Nigeria, zaidi ya watu Elfu sita wamekimbia makazi yao kufuatia shambulio baya lililofanywa na watu wenye silaha mwishoni mwa juma katika jimbo la Benue, ambapo zaidi ya watu mia moja wanahofiwa kufariki, shirika la dharura limesema.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Watu wenye silaha walishambulia kijiji cha Yelewata siku ya Ijumaa usiku, katika eneo ambalo limeshuhudia kuongezeka kwa ghasia, huku kukiwa na mapigano kati ya wafugaji wa Kiislamu na wakulima – wengi wao wakiwa Wakristo, wanaongangania ardhi na rasilimali zingine.

Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Dharura limesema zaidi ya nusu ya waliokimbia makazi yao, wengi wao wanawake na watoto, wanahitaji chakula, vitu vya kibinafsi, maji ya kunywa na vifaa muhimu vya matibabu.

Gavana wa jimbo la Benue amesema idadi ya waliofariki imefikia 59, ingawa shirika la Amnesty International linasema idadi hiyo inaweza kuzidi 100.

Rais Bola Tinubu alisema katika taarifa Jumapili usiku kwamba, ameagiza vyombo vya usalama kuchukua hatua madhubuti na kuwakamata wahusika wa vitendo hivyo.

Papa Leo XIV alilaani mauaji hayo wakati wa sala yake ya Jumapili huko Roma, na kuyataja kuwa “mauaji ya kutisha” ambapo raia wengi waliokimbia makazi yao waliuawa kwa ukatili wa kupindukia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *