Nigeria: Waombolezaji 15 wameuawa na watu wenye silaha Borno Nigeria

Wanajihadi wanaoshirikiana na kundi la Islamic State, wamewauwa waombolezaji 15 baada ya kuwapiga risasi, wakiwa msibani katika jimbo la Borno, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limeripotiwa kutokea siku ya Jumatatu, ikiwa ni mwendelezo ya mashambulio yanayowalenga raia wa kawaida, ambayo yameongezeka katika siku za hivi karibuni.

Wanajihadi kutoka kundi la Islamic State eneo la Afrika Magharibi (ISWAP), walivamia kijiji cha Kwaple, karibu na mji wa Chibok, wakiwa kwenye pikipiki na kuanza kuwapigisa risasi waombolezaji waliokusanyika kwenye msibani huku wengine wakipigwa risasi, walipojaribu kutoroka.

Wiki iliyopita, watu wengine zaidi ya 50 waliuawa baada ya kupigwa risasi, na watu wenye silaha na kuzua wasiwasi katika jimbo la Borno.

Eneo la Chibok, limeendelea kugongwa vichwa vya Habari kutoka na utovu wa usalama, hasa 2014 wakati, wanafunzi zaidi ya 200 walipotekwa na magaidi wa Boko Haram.

Licha ya wanajeshi wa serikali kupiga kambi katika mji wa Chibok, kwa zaidi ya miaka 10 sasa, utovu wa usalama umeendelea kushuhudiwa, ikiwemo kuuawa kwa wakulima 14 katika wilaya ya Gwoza wiki iliyopita, katika mpaka wa Nigeria na Cameroon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *