Nigeria: Wanajihadi wanatumia TikTok kuwasajili watu kujiunga nao

Wanajihadi kaskazini mwa Nigeria wanatumia mitandao ya kijamii kuendeleza kampeni zao kuwasajili wapiganaji wapya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Karibia watu 100 waliuuawa katika masururu mpya ya mashambulio ya mpya mwezi Aprili peke.

Kulingana na gavana wa jimbo la Borno, eneo ambalo limekabiliwa na utovu wa usalama tangu mwaka wa 2009, makundi yenye silaha yameendelea kuimarisha shughuli zake katika jimbo hilo la Borno.

Wanajidi wanatumia mitandao kama vile TikTok kuwashawishi watu kujiunga nao kwa kuonyesha silaha pamoja na pesa.

Watu wenye silaha wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya raia Kaskazini mwa Nigeria.
Watu wenye silaha wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya raia Kaskazini mwa Nigeria. REUTERS – Christophe Van der Perre

Makundi ya kihalifu yanayotekeleza mashambulio kwenye vijiji na kuwateka watu kwa ajili ya kikombozi kaskazini mwa Nigeria, yameripotiwa kutumia mtandao wa TikTok awali.

Licha ya kwamba akunti nyingi za makundi hayo kwenye TikTok zimefungwa, hatua ya baadhi yao kwenda moja kwa moja imekuwa mojawapo ya tatizo katika kuyakabili makundi hayo.

Msemaji wa TikTok alisema imekuwa vigumu kuweka wazi ni akaunti ngapi zinazohusishwa na makundi ya kijihadi zimefutwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *