
Takriban watu 19 waliuawa na watu wenye silaha katika shambulio kwenye eneo la uchimbaji madini ya dhahabu katika jimbo la Zamfara, kaskazini-magharibi mwa Nigeria, afisa wa chama cha wachimba madini na Amnesty International wameliamia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa, Aprili 25.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Majambazi walivamia eneo la uchimbaji madini mchana na kuua watu 19, wakiwemo wanamgambo watano waliokuwa wakilinda usalama kwa wachimbaji hao,” amesema kiongozi wa chama cha wachimba madini Yahaya Adamu Gobirawa. Mkurugenzi wa Amnesty International Nigeria, Isa Sanusi, ametangaza idadi ya waliofariki kuwa 20 katika kijiji “raia waliohama” cha Gobirawar Chali.
Kulingana na kiongozi wa chama cha wafanyakazi Yahaya Adamu Gobirawa, wachimba migodi 14 waliuawa papo hapo, huku wanamgambo watano wa usalama pia wakipoteza maisha. “Majambazi hao walishambulia eneo hilo saa sita mchana siku ya Alhamisi. Walirudi kwa wingi zaidi na wakiwa na silaha nzito baada ya jaribio la kwanza kuzimwa siku ya Jumanne,” amesema.
Amnesty International imeripoti idadi kubwa zaidi ya vifo, ikisema miili 20 imetambuliwa, baadhi yao walikufa kutokana na majeraha baada ya shambulio hilo. “Kijiji sasa hakina watu,” ameongeza Isa Sanusi, mkurugenzi wa Amnesty nchini Nigeria.
Eneo lililokumbwa na ghasia kutoka kwa makundi yenye silaha
Zamfara ni mojawapo ya majimbo yaliyoathiriwa zaidi na ukosefu wa usalama nchini humo. Kwa miaka kadhaa, makundi yenye silaha yamekuwa yakiongeza mashambulizi dhidi ya raia, vikosi vya usalama na maeneo ya kiuchumi. Makundi haya, ambayo mara nyingi hujulikana kama “majambazi,” huteka nyara ili kupata fidia, hupora vijiji, na kuchoma nyumba baada ya kuvipora.
Kiongozi wa chama hicho anashuku kuwa makundi haya yalishambulia mgodi huo kwa sababu hawakuhusishwa na uchimbaji madini. Mwaka jana, serikali katika eneo hilo ilituma kikosi cha “walinzi wa jamii” 5,200 ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.