Nigeria kuandamana leo kupinga ongezeko la gharama za maisha

Wananchi wa Nigeria leo Jumanne wamepanga kufanya maandamano mapya kulalamikia ongezeko la gharama za maisha. Maandamano hayo yaliyopewa jina la “Oktoba Mosi Bila Hofu” yamepangwa kwenda sambamba na kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa Nigeria.