Nigeria: Ghasia zimekuwa zikiongezeka kote nchini kwa wiki kadhaa

Katika muda wa wiki tatu zilizopita, takriban watu 250 wameuawa katika mashambulizi tofauti kote nchini Nigeria. Mara nyingi taratibu zilizotumliwa zinafanana: makundi ya watu wenye silaha hufyatua risasi. Hivyo kuua raia katika jamii za vijijini. Hasa katikati ya migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Lakini pia mashambulizi ya kigaidi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Abuja, Moïse Gomis

Kuibuka kwa kundi jipya la wahalifu, “Mahmuda”, kumefanya hali ya usalama kuwa ngumu. Hadi wakati huo, sehemu ya kati-magharibi mwa nchi inaonekana kuathiriwa kidogo na mauaji haya ya umati.

Siku ya Alhamisi hii, Aprili 17, Jimbo la Benue, Kaskazini-Kati mwa Nigeria, lilikubwa na mauaji ya watu 56 katika wilaya za Logo na Ukum. Siku moja kabla, tarehe 16 Aprili, kundi jipya la watu wenye silaha, Mahmuda, liliua watu 15 katika shambulio huko Kemaanji, kutoka jamii ya Kaiama. Eneo maarufu kwa uzalishaji wake wa shea katika Jimbo la Kwara, Magharibi ya Kati.

Mahmuda pia wanasemekana kuchukua udhibiti wa maeneo katika wilaya za Babana na Wawa katika Jimbo la Niger, ambalo bado liko katika ukanda wa kati wa Nigeria. Katika eneo la Hong la Jimbo la Adamawa kaskazini-mashariki, Boko Haram waliwaua watu saba mnamo Aprili 15, kwa kutumia vilipuzi.

Hapo awali, kati ya Aprili 3 na 10, karibu watu ishirini waliuawa na makundi yenye silaha huko Otukpo na Gwer katika Jimbo la Benue. Katika hali hii mbaya, Jimbo la Plateau lilikumbwa na hali mbaya zaidi. Kuanzia Machi 27 hadi Aprili 2, wanamgambo wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wafugaji walisababisha vifo vya watu wasiopungua 113 katika wilaya sita za Bokkos na Bassa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *