
Niger imetangaza siku ya Jumatatu, Machi 17, kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Francophonie (OIF). Niamey ilisimamishwa katika shirika hilo miezi michache baada ya mapinduzi yaliyompindua rais mteule Mohamed Bazoum mwezi Julai 2023. Kulingana na OIF, Burkina Faso “tayari imetangaza mbinu kama hiyo.”
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Katika barua iliyotumwa kwa wanadiplomasia walioko Niamey, Wizara ya Mambo ya Nje ya Niger imetangaza kujiondoa kwa nchi hiyo kutoka Shirika la Kimataifa la Francophonie (OIF).
Huu ni uamuzi wa “huru”, barua inabainisha.
Nchi jirani ya Burkina Faso tayari imefanya uamuzi “kama huo”, Oria K. Vande Weghe, msemaji wa Shirika la Kimataifa la Francophonie, amesema Jumatatu jioni kwenye telrvisheni ya TV5 Monde.
Niger na Burkina Faso, zote zikiwa zinaongozwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi, ni wanachama wa Muungano wa Nchi za Sahel, huku nchi ya tatu, Mali, ikitaraji kutoa uamuzi kuhusu suala hilo hivi karibuni. Nchi hizi tatu hazifichi nia yao ya kujiweka mbali zaidi na Ufaransa, ukoloni wa zamani.
Mali, Niger na Burkina Faso zilisimamishwa kutoka kwa shirika hilo baada ya mapinduzi yaliyowatimua malakani marais waliochaguliwa kidemokrasia. Nchi hizi tayari zilivunja ushirikiano wao wa kijeshi na Ufaransa kwa kuomba kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa katika ardhi zao.
Shirika la Kimataifa la La Francophonie ambalo liliundwa mnamo mwaka 1970, linaleta pamoja nchi 93 au serikali. Inazipa nchi wanachama wake usaidizi katika kuunda au kuunganisha sera zao na kutekeleza sera za kimataifa na hatua za ushirikiano wa kimataifa, kwa mujibu wa dhamira zake kuu kama vile kukuza lugha ya Kifaransa na anuwai ya kitamaduni na lugha