
Ni miezi miwili tu iliyopita nchini Niger. Usiku wa Januari 13 kuamkia 14, 2025, Waziri wa zamani wa Mafuta “alitekwa nyara” kutoka nyumbani kwake na wanaume waliovalia kiraia na kupelekwa kusikojulikana. Moustapha Barké yuko wapi sasa? Swali linaulizwa na wanasiasa na mashirika ya kiraia nchini Niger, ambao hawajapata habari kwa miezi miwili.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Ni hali mbaya sana,” mmoja wa wanaharakati wa mashirika ya kiraia anaelezea masikitiko yake. Hii ni hali isiyokuwa ya kawaida ambayo ni sawa na kutoweka kwa lazima na inapaswa kuwatia wasiwasi raia wote wa Niger, anaongeza.
Usiku wa Januari 13 kuamkia 14, 2025, wanaume waliovalia kiraia walikuja nyumbani kwa Moustapha Barké. Walifanya msako, wakauliza maswali, kabla ya kumpeleka waziri huyo wa zamani wa mafuta kusikojulikana. Tangu wakati huo, hajatokea tena. Yuko wapi kwa sasa? Je, ni anashtumiwa nini? Kufikia sasa, hakuna viongozi wote ambao tumefikia wameweza kutoa jibu kwa maswali haya.
Moustapha Barké ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha kiongozi wa upinzani Hama Amoudou cha Moden Fa Lumana, alikuwa mkurugenzi wake wa kampeni kwa uchaguzi wa mwaka 2021 Yeye yuko karibu na Waziri Mkuu wa sasa, Ali Mahaman Lamine Zeine. Alijiunga na serikali iliyoundwa baada ya mapinduzi ya mwezi wa Julai 2023 kama mkuu wa wizara kuu ya Nishati, Madini na Petroli. Majukumu yake yalipunguzwa baadaye, na alishikilia wizara ya mafuta kabla ya kufutwa kazi mwaka mmoja baadaye, mnamo mwezi wa Agosti 2024.